Header Ads

Baba mzazi wa Jose Mourinho amefariki, kuzikwa leo Ureno


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewasili nchini kwao Ureno kwa ajili ya shughuli ya mazishi ya baba yake mzazi mzee Jose Manuel Mourinho Felix ambaye amefariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 79 baada ya miezi kadhaa ya kuugua.
Mourinho alionekana akiwasili Setubal akiwa na rafiki zake na familia yake Jumatatu baada ya taarifa za kifo cha baba yake mzazi ambaye atazikwa  leo Jumanne.
Enzi za uhai wake na maisha ya soka, Mourinho Felix alikuwa mlinda mlango wa klabu za Vitoria Setubal kisha Belenenses akicheza mechi 274 za Ligi Kuu ya Ureno kati ya 1955 na 1974 huku akicheza mara moja pekee kwenye timu ya Taifa la Ureno akitokea kwenye benchi mchezo dhidi ya Jamhuri ya Ireland mwaka 1972.
Baada ya kustaafu soka Mourinho Felix alikuwa kocha wa klabu kadhaa za Ureno zikiwemo Uniao Leiria, Amora, Rio Ave, Belenenses na Vitoria.
Mourinho akiwa kwenye picha ya pamoja na baba yake Felix, ambaye alicheza zaidi ya michezo 250 kwenye Ligi Kuu ya Ureno
Baada ya taarifa za kifo cha baba yake Mourinho alipost picha hii kwenye Instagram yake
Felix, ambaye alisumbuliwa na maradhi kwa miezi kadhaa alifariki Jumapili
Mourinho na familia yake pamoja na rafiki zake wakielekea Kanisani kwa ajili ya shughuli za mazishi ya Felix
Mourinho (wa pili kushoto) akisindikizwa na familia akiwepo binti yake Matilde (wa pili kulia) kuelekea kwenye msiba wa baba yake
Jose Mourinho akatiwa moyo na mmoja wa rafiki zake kufuatia kifo cha baba yake mzazi aliyefariki Jumapili

No comments:

Powered by Blogger.