ALICHOJIBU SHETTA BAADA YA KUMSIKIA SHABIKI REDIONI KUHUSU ALIKIBA NA DIAMOND
MuroTv
Burudani
Alichojibu Shetta baada ya kumsikia shabiki Radioni kuhusu Alikiba na Diamond
Kauli ya Shetta imekuja baada ya kuulizwa swali la moja kwa moja na mmoja wa mashabiki wake kupitia kipindi hicho ambaye alitaka kujua yuko upande upi kati ya zinazotajwa kuwa team za mastaa Alikiba na Diamond platnumz.
Shetta amesema hana team na haamini kama kuna team baina yao lakini amedai kuwa anawakubali wote kwa kuwa ni wasanii wenzake na marafiki zake pia:>>>“Mimi sina team bro, mimi ni team Shetta hao wote ni washikaji zangu, wasanii wenzangu na ndugu zangu…kwanza kuna ma-team? Sijui kama kuna team ila mimi team Shetta” – Shetta.
Mbali na hayo, Shetta ametoa ahadi kwa mashabiki wake akisema atawaletea wimbo mpya hivi karibuni ambao tayari video yake ameifanyia Dubai ambako alikuwa na show akiahidi kuutoa mwisho wa Mfungo wa Ramadhani video na Audio.

No comments:
Post a Comment