ZANZIBAR YADHIBITI UCHIMBAJI MCHANGA
MuroTv
Zanzibar yadhibiti uchimbaji mchanga
31 Mai 2017
Mohamed alitoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupinga hatua ya Serikali kuratibu kazi za uchotaji wa mchanga katika machimbo ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema Serikali haina nia ya kupora mali ya mtu lakini kilichofanyika ni kudhibiti na kusimamia uchotaji huo wa mchanga baada ya kutokea kwa athari mbalimbali. Kwa mfano alisema katika kipindi ambacho wananchi walikuwa wakiratibu wenyewe, athari kubwa za kimazingira zilijitokeza.
Alizitaja athari hizo kuwa ni baadhi ya maeneo yaliyochotwa mchanga kutofaa tena kwa kilimo ambapo wakulima wengi wanalalamikia kukosa chakula cha kutosha. Alisema maeneo hayo hayafai kwa kilimo kwa sababu mchanga umechotwa bila maelekezo ya kitaalamu ikiwemo kwenda chini zaidi na hivyo kuondoa rutuba ardhini.
Alisema athari za kimazingira zimechangia maji chumvi kuingia katika mabonde hayo na kusababisha mmomonyoko wa ardhi. Alisema athari hizo ndizo zilizosababisha Serikali kuchukua jukumu la kuratibu kazi za uchotaji wa mchanga na si kufanya biashara. Zanzibar ina uhaba mkubwa wa mchanga kiasi cha kuweka utaratibu mzuri wa udhibiti wake ikiwemo kuendesha biashara hiyo.

No comments:
Post a Comment