Header Ads

TRUMP: IRAN HAITARUHUSIWA KUMILIKI SILAHA ZA NYUKLIA

MuroTv 

Dira ya Dunia

Trump: Iran haitaruhusiwa kumiliki silaha za nyuklia

Donald Trump (kushoto) na Benjamin Netanyahu wakiwa na wake zao uwanja wa ndege wa Tel Aviv tarehe 22 Mei Rais wa Marekani Donald Trump ameanza ziara yake nchini Israel kwa kuonya kuwa kuna tisho kutoka nchini Iran ikiwa itamiliki silaha za nuklia.

"Iran haitaruhusiwa kamwe kumiliki silaha za nuklia," Trump aliwaambia waandishi wa habari.

Alisafiri kutoka nchini Saudi Arabia, mshirika mkubwa wa Marekani ambapo alitoa hotuba kwa viongozi wa kiislamu.
Bw Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina katika kipindi cha siku mbili atakazokuwa eneo hilo.
 Trump alizuru ukuta wa magharibi ambalo ni eneo takatifu
Rais huyo amesema kupatikana kwa mkataba wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina yatakuwa mafanikio makubwa, lakini hakusema mkataba kama huo unafaa kuchukua mwelekeo gani.
Amesema angependa sana pande zote mbili ziamue kuhusu mkataba huo wa amana kwa mashauriano ya moja kwa moja.
Katika mkutano mkuu wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu mjini Rihadh siku ya Jumapili, Bw Trump aliwataka viongozi hao kuwa kwenye mstari wa mbele katika kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu na wapiganaji wenye itikadi kali na "kuwafurusha kutoka kwenye dunia hii."
  • Wakili: Mwana wa Muhammad Ali alizuiliwa kuingia Marekani
  • Marufuku mpya ya Trump yazuiwa Marekani
Aliitaja moja kwa moja Iran na kusema kwamba imekuwa "ikichochea mizozo ya kidini na ugaidi" katika kanda hiyo kwa miongo mingi.
Bw Trump pia alikariri tena kwamba anaamini amani kati ya Waisraeli na Wapalestina inaweza kupatikana.
Rais huyo wa Marekani amekuwa akichukuliwa sana kuwa muungaji mkono mkubwa wa Israel kuliko mtangulizi wake Barack Obama.

No comments:

Powered by Blogger.