POLISI UINGEREZA WALALAMIKIA PICHA ZA MANCHESTER
MuroTv
Dira ya Dunia
Polisi Uingereza walalamikia picha za Manchester
Polisi nchini Uingereza wameyalaumu machapisho yaliyotolewa katika gazeti la New York Times juu ya picha na taarifa kutoka katika eneo ambalo shambulio la bomu lilitokea mjini Manchester.
Maafisa nchini humo wanasema kuvuja kwa picha hizo kuna haribu uchunguzi wa polisi na kuondoa imani na washirika wao katika masuala ya kiintelejinsia.Picha hizo zinaonesha vitu mbalimbali ambavyo vingetumika kama ushahidi kama vile betri na vitu vingine vyenye muonekano wa vilipuzi.
- Mshukiwa wa shambulio la Manchester atajwa
- Shambulizi la Manchester: Tunafahamu nini?
Waziri mkuu wa Uingereza anatarajiwa kulipeleka suala hilo kwa Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuia ya NATO, ambao unafanyika leo.
No comments:
Post a Comment