SIMBA YAKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA IKIMTAJA RAIS WAO KUGOMEA ZAWADI YA MSHINDI WA PILI
Michezo
Simba SC imekanusha taarifa inayosambazwa ikimtaja Rais wao


Leo May 25 2017 ziliripotiwa habari za uongo katika mitandao ya kijamii kuwa wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa Rais wao Evans Aveva wamekubali nafasi ya mshindi wa pili na kufuta malalamiko yao FIFA kuhusiana na TFF kuituhumu kutotenda haki.
Simba imekanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wao wa instagram “Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba Sports Club tunawaomba mpuuze ujumbe huo unaosambazwa. Uongozi wa Simba haujatoa taarifa hio”
No comments:
Post a Comment