Header Ads

RAIA WAKUMBWA NA HATARI KUBWA MOSUL, IRAQ.

MuroTv

Dira ya Dunia

Raia wakumbwa na hatari kubwa Mosul, Iraq

Wanajeshi wanasema kuwa wamepiga hatua kwa saa chache wanapojaribu kuwatimua wanamgambo Huku vita kati ya serikali ya Iraq na wapiganaji wa Islamic state vikiendelea kushika kasi mjini Mosul, raia waliokwama katika mji huo watakabiliwa na majanga makubwa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Kulingana na Mratibu wa misaada ya kibinadam wa umoja huo, Lise Grande, raia wa Mosul wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, maji, dawa na umeme.
  • Majeshi ya Iraq yasonga mbele Mosul
Rai wakwama Mosul huku mapigano yakiendelea
Raia wanaojaribu kutoroka wanauwawa na Islamic state.
Kumeibuka ripoti kwamba walenga shabaha wa Islamic state wamekuwa wakiwauwa watoto kimakusudi.
Wanajeshi wanasema kuwa wamepiga hatua kwa saa chache wanapojaribu kuwatimua wanamgambo hao kutoka ngome zao za mwisho katika mji wa zamani wa Mosul.
  • Marekani kuanzisha uchunguzi kwa mashambulizi ya Mosul
Maelf ya raia wameukimbia mji huo wa kaskazini tangu jitihada za kuukomboa zianze mwezi Oktoba mwaka uliopita.
 Mapigano yamesababisha kuhama zaidi ya watu 500,000

No comments:

Powered by Blogger.