MICHEZO
Michezo
KALI KULIKO: Kituko kingine cha Mourinho…mkutano sekunde 10?

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ambaye anatajwa kuwa na matukio alifanya kituko cha kufungia msimu wa English Premier League baada ya kufanya mkutano wa baada ya mechi uliodumu kwa sekunde 10 kwa sababu hakuulizwa maswali.
Mourinho alitakiwa kukutana na waandishi wa Habari kufuatia ushindi wa Manchester United wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa mwisho wa msimu wa EPL 2016-2017 uliopigwa Old Trafford.
Baada ya kuingia kwenye mkutano huo ambao pia haukuwa na watu wengi hakuna mtu ambaye aliuliza swali lolote hivyo Mourinho akasema: “Kwa herini” kisha akaondoka.
Awali akifanya interview na Televisheni ya Klabu ‘MUTV’ Mourinho alisema: “Msiniulize mambo mengi kwa sababu najua niko kwenye fainali.”
Mshuhudie kwenye hii video hapa chini kwa kubonyeza play!!!
Mourinho alitakiwa kukutana na waandishi wa Habari kufuatia ushindi wa Manchester United wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa mwisho wa msimu wa EPL 2016-2017 uliopigwa Old Trafford.

Mourinho akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ambao haukuwa na watu wengi baada ya mechi ya Manchester United vs Crystal Palace
Awali akifanya interview na Televisheni ya Klabu ‘MUTV’ Mourinho alisema: “Msiniulize mambo mengi kwa sababu najua niko kwenye fainali.”

Muongozaji wa mkutano akiwauliza wanahabari kama wana maswali kwa Mourinho

Baada
ya kusubiri kwa sekunde sita bila kuulizwa swali, Mourinho akasema ‘kwa
heri’ na kutoka chumba cha mikutano sekunde 10 baada ya kuingia
“Hatukutaka kutoa heshima kwa wapinzani wetu” – Kocha Serengeti Boys
No comments:
Post a Comment