Trump 'kupigania amani'' baada ya kukutana na Papa
DUNIANI
Trump 'kupigania amani'' baada ya kukutana na Papa
Mai 25, 2017
Rais Donald Trump ameapa kutumia
wadhfa wake ili kukuza amani baada ya kile alichokitaja kuwa mkutano
muhimu na Papa Francis mjini Vatican.
Katika chapisho la mtandao
wake wa Twitter baada ya viongozi hao wawili kukutana, bwana Trump
alisema kuwa ni heshima kubwa katika maisha yake kukutana na kiongozi
huyo wa kanisa katoliki na kwamba amepata ari na azma ya kupigania amani
duniani.Wawili hao hapo awali walitofautiana vikali katika maswala kama vile Uhamiaji, hali ya hewa, na ujenzi wa ukuta wa Mexico.
- Papa Francis ataka mazungumzo kuhusu Korea Kaskazini
- Kiongozi wa Palestina akutana na Papa Francis
- Donald Trump amwalika rais wa Palestina Mohamud Abbas
- Biden atokwa na machozi akipewa medali
Donald Trump alitaja matamshi hayo kama yasio na heshima.
Rais Trump sasa amewasili mjini Brussels kwa mazungumzo na Nato na maafisa wa EU.


No comments:
Post a Comment