MAGUFULI AKARIBISHA WAWEKEZAJI ZAIDI CHINA
Rais Magufuli akaribisha wawekezaji zaidi China
Rais wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.
Dk Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF na Mbunge wa Bunge la Wananchi wa China, Zhan Xin.
Rais Magufuli alisema Tanzania imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati kati ya 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia megawati 10,000 na ili kufikia malengo hayo, wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama vile gesi, makaa ya mawe na jua.
“Kwa hiyo, Ndugu Zhang Xin kawaambie wawekezaji wenzako wa China waje Tanzania, nchi zetu ni ndugu na marafiki wa miaka mingi, itakuwa jambo jema wakija kuunga mkono juhudi zetu za kujenga viwanda kwa kuzalisha umeme mwingi na pia kushiriki katika miradi mingine ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara,” alisema Rais Magufuli.
Wakati huo huo, Rais John Magufuli jana alikutana na Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak na viongozi hao walizungumzia utekelezaji wa mambo mbalimbali ya ushirikiano na miradi ya maendeleo iliyotokana na makubaliano ya mkutano wa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Magufuli jana alikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini, Yunus Belet na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Korea, Songwon Shin.

No comments:
Post a Comment