Fahamu kuhusu Mnyama mkubwa zaidi Duniani 'NYANGUMI'
Habari
ndugu msomaji wa Muro TV na murotv.blogspot.com. Natumaini u mzima wa afya leo nimekuandalia
makala fupi maalumu kwa ajili ya kumzungumzia samaki mkubwa zaidi
duniani na pia ndiye mnyama mkubwa zaidi duniani, si mwingine huyu
anaitwa NYANGUMI.
Nyangumi
ni moja ya viumbe wanaoishi baharini kwenye kina kirefu sana. Mnyama
huyu anasadikika kuwa mwanzoni aliishi nchi kavu miaka milioni iliyopita
ila kutokana na mabadiriko ya tabia ya nchi aina hii ya wanyama
wakahamia majini. Mnyama huyu anamaajabu mengi sana ambayo hakuna kiumbe
hata mmoja mwenye tabia kama zake ndomana amejibebea sifa ya kuwa
mnyama mkubwa zaidi duniania.
1. UZAZI WA NYANGUMI
Nyangumi hubeba ujauzito kwa muda wa miezi 10-12, mtoto wa wale akizaliwa anakuwa na Tani 5.5 mpaka 7.3 na urefu wa Mita 7.5. Mtoto wa Nyangumi hunyonya Lita 223 kwa siku na huongezeka kilo 3.4 kila baada ya lisaa yaani dakika 60 mpaka afikishapo miezi 8. Nyangumi hubarehe pindi afikishapo miaka 10-15.
2. UMBILE LA NYANGUMI
Nyangumi mkubwa ana Tani 144 amabzo ni sawa na uzito wa wanaume 2000.
Ukiachana na hilo ulimi wa nyangumi unauzitosawa na Tembo aliyezeeka
amabapo wachezaji wa mpira wa timu mbili wanaweza kusimama juu ya ulimi
wake. Nyangumi mkubwa zaidi alipatikana kwenye bahari ya Atlantic amabapo alikua na urefu wa Mita 30.5.
3. UMRI
Nyangumi mkubwa zaidi anasadikika kuishi kwa miaka 200
TAZAMA VIDOE (MAAJABU YA NYANGUMI)
No comments:
Post a Comment