Mr Nice kafunguka na kusema ‘Sijutii chochote, vitu vyote nimeshafanya’ (+Audio)
Mwimbaji na muasisi wa style ya TAKEU kwenye Bongofleva Mr Nice ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akiishi Kenya lakini sasa amerudi Tanzania na kukiri mara kadhaa kuzushiwa kifo, ingawa hafanyi tena muziki kwa sasa amefunguka kuwa hajutii maisha anayoishi.
Mr Nice ambaye kwa sasa anachukua headline baada ya kuonekana kwenye video ya wimbo wa ‘Sina’ wa mwimbaji Harminize alikuwa kwenye The Weekend Chart Show ya Clouds TV July 28, 2017 na kusema hajutii chochote huku akiwapa ushauri wasanii wa sasa.
>>>”Sijutii, hakuna kitu chochote najutia. Kuhusu majuto kwa Mr Nice sahau. Mimi vitu vyote nimeshafanya hata ungenifanya nini mimi ni huyu huyu nitaendelea kuwa huyu hakuna kitu najutia kabisa.
“Mimi nadhani kitu cha muhimu kuzingatia kwa wasanii wenzangu ni upendo. Waache unafiki wajue kuna leo na kesho. Wanapopata, wajue kuwekeza maana unajua watu wanaongea mengi mara Mr Nice hela zake amezitumia sana lakini watu hawajui ninavyovimiliki.
“Wanaona naganga sasa hivi lakini hawajui ni hela ile ile mliyonipa ndio mpaka sasa hivi. Huko niliko inaniongezea zaidi bado kwa nyimbo zile zile. Ndio maana Wakenya wanasema hawana haja na nyimbo zangu mpya wanasema wanataka ile ile Fagilia.
“Waheshimiane na wafanye kazi kwa bidii maana muziki unaenda juu halafu unashuka chini. Kwa hiyo, hata kama kuna msanii yupo juu kuliko wengine kama wanavyojiona wao, wasiamini hilo kwa sababu saa yoyote mambo yanabadilika hata Ulaya.
“Inawezekana wengine wakaja kuwa juu zaidi yangu unajua unafanya muziki lakini unaangalia na waliotutangulia, iwe Bongo au wapi ukiwauliza mwanamuziki gani unamkubali atasema Mr Nice. Ndio maana na mimi ukiniuliza nani unamkubali namba moja nitasema mimi. – Mr Nice
SIKILIZA SHILAWADU WALIVYOMNASA
No comments:
Post a Comment