Header Ads

Je, ni kweli Diamond anafanyiwa Figisu ili ashuke Kimuziki au yeye ndo Tatizo?



Udakutz
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa mashabiki wa WCB wakidai kuwa Diamond pamoja na Team yake anafanyiwa figisu na watanzania ili ashuke na sababu kibao..Je hizi stori zina ukweli au ni ndo mfa maji haishi kutaptapa.

To my side pamoja na kuwa ni shabiki wa WCB sioni kama ni kweli Diamond anafanyiwa figisu ila yeye ndo anasababisha haya naweza nikatoa sababu mbili tatu za kuunga hoja:

1.SHOW OFF
Hichi ndo kitu namba kinacho muangusha Diamond pamoja na Team yake. Diamond amekuwa mtu wa show off sana kila kitu anachofanya kiwe cha siri au cha kawaida ambacho hakina umuhimu wowote ataposti kwenye kurasa zake za mitandao, hii inamshushia heshima kwa kasi sana.

2.UROPOKAJI NA KUDHALILISHA WANAWAKE
Hakuna watu wenye uwezo mkubwa wa kumfanya mwanamziki au msanii yeyote mahali popote awe star zaidi ya wanawake, wanawake wana nguvu kubwa sana kwenye sanaa kwa ujumla. Sasa mshikaji wangu baada ya kumpata huyu bibi wa kiganda anawaona wanawake wote wa kibongo kama mashudu tu vile, na kuonyesha dharau za waziwazi kwa mfano kitendo cha kumwita hamissa mobeto "Bitch" kimeudhi watu wengi sana na mimi pia nikiwemo.

3.KUTAKA ASIKIKE YEYE TU NA WASANII WAKE.
Kitendo cha Diamond kutoa wimbo masaa machache baada ya mpinzani wake watu wengi wamektafasli kama ni ushamba na kutokujiamini na kutaka asikike yeye tu kuliko wasanii wengne. Watanzania tunatamani kuwepo na kundi kubwa la wasanii waliotoboa international sasa inapotokea kuzibiana riziki kwa kweli hili halikubaliki...

4.KUMUWAZA SANA MSHINDANI WAKE (KIBA) KULIKO UBORA WA KAZI.
Zamani Diamond alikuwa anatoa nyimbo nzuri tu na alikuwa hatumii nguvu nyiiingi kuzipromote hii ni kwa sababu alikuwa anatumia muda mwingi kuziandaa kwa umakini mkubwa lakini tokea beef lianze naona linamuchanganya sana inaonekana anatumia muda mwingi sana kumuwaza mpinzani wake kuliko ubora wa kazi. Na siku Mondi ukiacha kumuwaza Kiba ndo siku atakayokuwa huru na ataanza kutoa nyimbo nzuri zilizokamilika siyo hizi liipua lipua anazotoa siku izi

Maoni yako yanakaribishwa huo juu ni mtazamo wa  Kifimbocheza Nini Mtazamo wako?

No comments:

Powered by Blogger.