ANGALIA PICHA | JUMLA NA JINSI RISASI ZILIVYOMPATA TUNDU LISU
Na Mr Muro
Mbunge
wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.
Selasini
amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari
tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia.
Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.
"Hao
watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona
kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha
risasi upande wa Lissu." amesema
Selasini ame,sema “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."
Lissu amepigwa risasi jana Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadae mida ya saa sita usiku alipelekwa Nairobi kwa ndege ya kukodi kwaajili ya kupata matibabu zaidi na usalama pia wa maisha yake.
Tundu Lisu alipata mashambulizi ya Risasi akiwa ndani ya gari hili na huu ni muonekano wa baadhi ya Risasi zinazoonekana kwa mbali baada ya mashambulizi hayo makali
Gari aliyokuwa amepanda Mh Tundu Lisu inaonyesha Jumla ya Risasi 25 zilirushwa upande wa Tundu lisu
Risasi 4 zilimpata Mh Tundu Lisu Miguuni ikiwa ni Risasi 2 kwa kila mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu, Jumla ya Risasi zilizompata haijafahamika bado lakini mwanzo ilisemekana ni Risasi 5 ndio zilimpata (kwa maelezo ya mwanzo | Risasi 2 miguuni, 2 Tumboni na 1 mkononi) na baadae kusemekana ni Risasi 20 ndio zilizompataMuro TV na murotv.blogspot.com zinzendelea kufatilia na Zitakujuza zaidi kila kitu kinachoendelea
-------Tupo karibu nawe------
No comments:
Post a Comment