Wema Sepetu Afunguka Haya Kuhusu Wahasimu Wake Kajala Masanja na Munalove
STAA
wa filamu mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa
mara ya kwanza kuwa hajawahi kuwakumbuka (kuwamis) waliokuwa mashoga
zake wa damu, Muna Alphonse ‘Muna’ na Kajala Masanja na kudai
alishawatoa kwenye akili yake.
Akizungumza na Star Mix, Wema alisema kuna baadhi ya watu ambao
hajaonana nao muda mrefu na anawakumbuka kila mara lakini kwa upande
wake hajawahi kuwakumbuka rafiki zake hao ambao huko nyuma walikuwa kama
kumbikumbi.
“Sitaki kusema dhambi jamani sijawahi kuwamisi hawa watu (Muna na Kajala) kabisa naona kama niliwafuta kwenye kichwa changu maana najikuta kuna watu nawakumbuka lakini hao hapana,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment