Hali ukumbi wa Bomas yabadilika matokeo yakisubiriwa
Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec amewasili Bomas |
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed na washirika wengine wakuu wa Rais Uhuru Kenyatta wamewasili Bomas.
Mabalozi wa Marekani na Uingereza pia wamewasili.
Kunashuhudiwa shughuli nyingi na usalama umeimarishwa pamoja na hali kuonekana kubadilika katika ukumbi huo.
Tume ya uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba inatarajia kupokea matokeo yote kutoka vituo vya kupigia kura kufikia leo saa sita mchana.
Mwenyekiti wa tume hiyo anatarajiwa kutangaza matokeo baadaye baada ya kuhakikiwa kwa fomu za matokeo.
Matokeo ya awali kwenye tovuti ya tume hiyo yanaonesha Rais Kenyatta akiongoza kwa takriban asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa dhidi ya Bw Odinga.
Tume ya uchaguzi ina siku saba kisheria kutangaza matokeo ya urais.
Gari likiwa linabeba zulia jekundu |
No comments:
Post a Comment