Header Ads

UCHAWI: Ardhi imejaa inatapika matapishi ya damu

Tokeo la picha la wachawi
ARDHI imebeba siri nzito sana watu wa kale wanajua, kwenye ardhi kuna kila aina ya uchafu, ardhi imebeba asili ya kila kitu kilichopo katika uso wa dunia, waganga wakitaka kufanya matambiko wanaitumia hii hii ardhi kuficha mambo yao, wachawi wakitaka kumfunga mtu asiendelee pia huifadhi uchafu wao na sadaka zao katika ardhi. ni ajabu sana wachawi wanatoa sadaka huku wacha Mungu wakishindwa kabisa kutoa sadaka kwa ajili ya Mungu wao.

Wachawi ni watu wabaya sana huwezi amini akikuchukia anadiliki kutoa sadaka ili akuangamize wengine wanadiliki kutoa sadaka za wanyama, damu za wanyama na muda mwingine ata damu za binaadam uhusika, hiyo yote ili ammalize binaadam mwenzake...ardhi ingekuwa inasema ingeongea mengi sana ya siri...ingeongea jinsi inavyoficha vitu vya watu waovu...si ajabu mchawi akauzika mguu tena mguu wa mtu aliehai...Mtu anatembea kumbe mwili wake kuna sehemu umezikwa.
[​IMG]
Si nia yangu kuumbua wachawi ila mambo wachawi wanayo yazika ardhini ni makubwa sana, ni rahisi sana mchawi kuzika karatasi yenye majina yako yote tarehe yako ya KUZALIWA na siku yako ya KUFA. kama humjui Mungu mchawi akifukia hicho kikaratasi pindi tarehe itapofika aliyoiandika ya wewe kukuondoa ulimwenguni hutochomoka wala kifo hutokikimbia utakufa tuu labda uanze kumrudia Mungu ili kuvunja LAANA zote za wachawi wanazokuwekea ilikukumaliza.
[​IMG]
Tumrudie Mungu uchawi ni kama kigonjwa kinachotumaliza kigonjwa ambacho tuna kipuuza ila
uchawi unatumaliza sana..tumrudie Mungu haswa ardhi inatapika. akili na mafanikio yetu yanafukiwa ardhi, mahusiano yetu hayadumu kumbe wachawi wameyazika ardhini, atua zetu njema zote zinafukiwa ardhini kila tunapoenda tunajikuta atufanikiwi kumbe waganda na wachawi wamefukia atua zetu ardhini.
na kikubwa kinachotumaliza kila wafanyacho waganga kinabaki kizazi hadi kizazi hivyo ni rahisi sana leo kuathiriwa na mambo waliyofungiwa mababu na mabibi zetu.
[​IMG]
Kama wachawi wanaweza kutoa sadaka ili watumalize basi na sisi tumrudie Muumba wetu tena tujitahidi katika kutoa sadaka ili tujikomboe maana wachawi wanaweza wasikuroge wewe ila kumbuka kuwa toka enzi za mababu uchawi ulikuwepo hivyo inawezekana mababu zetu walilogwa enzi hizo mimi na wewe leo tukapata tabu ambayo waliwahi kuipata babu zetu. tabu ambayo babu zetu walishindwa kuikomboa au kuitoa. SADAKA ina siri nzito sana.
[​IMG]
Tunatembea barabarani kumbe kuna wachawi walitulaani kwa vifungo walilaani mababu zetu, walifunga ukoo mzima, leo kila tunachofanya akifanikiwi, kila ukianza kazi unafukuzwa, watu wanakuchuki bila sababu maalum. tufanyeni toba tuondoe kila kilichofukiwa kwenye ardhi ili kuzuia maendeleo yetu mimi naanza kusema
''Ewe ardhi tapika kila kilichofukiwa kwa majina yangu tapika kila ulichokimeza, ardhi tapika mafanikio yangu, ardhi tapika baraka zangu, tapika kila laana waliyowekewa babu zangu na bibi zangu, ardhi tapika mafaniki ya ukoo wangu, ardhi tapika mafanikio ya marafiki zangu wote pamoja na mafanikio ya marafiki zangu wa humu murotv.com, ardhi tapika kila ulichomezeshwa na waganga wakakifukia kwenye ardhi leo ardhi tapika"
[​IMG]
''Ardhi tapika waganga wote wa kule kijijini na matambiko yao yote yatapikwe watolewe na kuondoka kabisa atuwataki, majini na uchafu wote wa kichawi utapikwe utoke kabisa ndani ya ardhi.

Ardhi sikia watoe wote watapike wote wenye nia ovu kwenye ardhi ya mtaani kwangu mkono wa mungu upite, wachawi wote, waganga wote, washirikina wote wanaotesa kwenye mtaa wangu watapikwe wote, na matunguli yao, na ibada zao mbovu zote ardhi tapika, wasiwange tena.Ardhi tapika na maradhi yote ya kurithi tuliyotupiwa na yakafukiwa ili yatutese" amin.
[​IMG]

No comments:

Powered by Blogger.