Biashara za kufanya Katika Buti ya Gari Lako
Maamuzi juu ya biashara gani ufanye ni magumu sana na mawazo mengi
mazuri ya biashara yanaishia hewani bila utekekelezaji kwa sababu ya
kukosa msukumo wa kuanza na kubadili mawazo mazuri kuwa vitendo.
Kuna biashara nyingi zenye faida ambazo zinaweza kufanyika nyuma ya buti ya gari.
Katika mada hii ninaelezea biashara za kufanya katika buti ya gari
ambazo kila mwenye gari anaweza kuzifanya kwa mtaji mdogo na bila
kuhitaji duka au chumba cha kuuzia.
Kwa wale wenye magari na wanafanya kazi za kuajiriwa biashara hizi
zinaweza kuwasaidia kuongeza kipato chao na kuboresha uchumi katika
familia zao
Wateja wa Biashara za Kufanya katika Buti ya Gari
Kama ilivyo kwa biashara yoyote ili ufanikiwe ni lazima uwe na bidhaa
na masoko,yaani uwe na wateja ambao wanahitaji bidhaa zako au huduma
unazotoa. Uwe na wateja wenye njaa au uhitaji kiasi kwamba watakuwa
tayari kununua bidhaa zako.
Kwa biashara za aina hii za kufanya nyuma ya buti ya gari, kwa kiasi
kikubwa wateja wako ni wafanyakazi wenzako au wateja wa kampuni
unalofanyia kazi wakiwemo makampuni shirika na kampuni yako.
Ukiachia wateja wa kazini, unaweza ukauza kwa wanachama wenzako
katika vikundi mbalimbali. Watu wengi ni wanachama katika makundi na
vyama mbali mbali kama vikundi vya kusaidiana,vikundi vya kikabila na
vikundi vya kuinuana kifedha na kibiashara.
Wateja wengine ni washirika katika imani kama makanisani na misikitini na sehemu nyingine za ibada.
Namna ya Kuuza Biashara Nyuma ya Buti ya Gari
Kutegemeana na aina ya bidhaa utakazouza,mpangilio na namna ya uuzaji
unaweza kutofautiana. Unaweza kuweka boksi na kuweka bidhaa humo
kwajili ya kuwaonesha wateja wako. Kwa bidhaa kama vipodozi au nguo,
kabati au boksi linaweza kufaa. Begi au briefcase linaweza kutumika kuoneshea bidhaa zako.
Pia unaweza kutengeneza sanduku la mbao na ukalinakishi vyema kutia
mvuto na ukatumia kuoneshea bidhaa zako nyuma ya buti la gari lako.
Unapotengeneza boksi ni muhimukutazingatia ukubwa wa buti lako.
Muda wa Kuonesha au Kuuza Bidhaa:
Unaweza kuuza bidhaa zako wakati wa asubuhi kabla ya kazi, wakati wa
mapumziko ya chai au chakula cha mchana na jioni watu wanapomaliza kazi.
Unaweza kukaribisha watu na kuwajulisha kwa njia ya ya programu za
mtandao lama facebook,twitter na whatsapp. Lakini unaweza kuongea nao
moja kwa moja,ana kwa ana.
Barua pepe inaweza kusaidia pia kusambaza ujumbe kwa watu unaowalenga kulingana na bidhaa yenyewe.
Si unajua, huwezi kulenga kila mtu kama unauza nguo za ndani za wanawake mfano au vipodozi vya nywele kwa mfano.
Bidhaa au Huduma Unazoweza Kuuza Kwa Biashara za Kufanya katika Buti ya Gari
Zifutazo ni baadhi tu ya biashara na bidhaa au huduma za kufanya katika gari lako:1. Nguo
Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza nguo katika buti ya gari. Unaweza
kuuza ngua mchanganyiko au nguo za aina moja. Mfano ya nguo za aina
moja ni kama magauni,nguo za ndani,mashati,suruali,nguo za
michezo,mashuka au mabranketi. Nguo mchanganyiko zinahusisha zote
zilizotajwa au baadhi yake.
2. Vitafunwa
Wafanyakazi wengi hununua vyakula kwajili ya nyumbani wakitoka kazini. Mfano mkate au mboga mboga ,nyama n.k. Unaweza kuanzisha biashara ya mikate na kuipaki kwenye sanduku nyuma ya buti la gari. Vitafunwa vingine ni keki,maandazi,sambusa na nyama au soseji.
3. Matunda
Unaweza kuuza matunda yasiyoandaliwa au yaliyo andaliwa tayari kwa kuliwa
Matunda yasiyoandaliwa ni kama machungwa
asiyomenywa,mananasi,mapapai,maembe. Kama unashamba lako binafsi
biashara hii inaweza kukuongezea kipato ambacho ungekosa kama usingeamua
kuuza.
Matunda yaliyoandaliwa yahusishwa kumenya matunda na kuyaandaa kwa
kuliwa. Mfano ni mchanganyiko wa maembe,papai na tikiti maji ambayo
yamekatwa vipande vidogo vidogo na kuwekwa katika vibakuli vyenye
vifuniko. Kwajili ya kuongeza ubora na kutunza ni vyema ukaweka katika
friji na kisha kutunza katika kitunza ubaridi ambacho unaweza kukiweka
katika buti ya gari lako.
4. Bidhaa za Elekroniki
Bidhaa nyingine unazoweza kuuza nyuma katika buti la gari ni zile za eletroniki kama simu,kompyuta mpakato,saa za mkononi,iPad na tableti za aina nyingine kama Samsung au nyinginezo.
5. Juisi za Matunda
Kama ilivyo kwa matunda,unaweza kukamua matunda ya aina moja au mchanganyiko nna kuviweka katika vikopo vyenye mifuniko na kuvipooza katika friji na kisha kuvipaki katika sanduku la kuhifadhi ubaridi ambalo utaliweka nyuma katika buti la gari lako.
6. Bidhaa za Watoto
Wazazi wanawapenda watoto wao na wako tayari kulipia bidhaa kwaajili yao. Hivyo bidhaa za watoto nimojawapo ya zile zinazouza sana. Unaweza kuuza bidhaa za aina moja kama chupi za mkojo (daipa),midoli ya kuchezea,mashati na suruali.
Au unaweza kuamua kuuza bidhaa za watoto za aina moja kama viatu au chupi pekee.
7. Vipodozi
Vipodozi na bidhaa za urembo zina soko kubwa hasa kwa wakinadada na akina mama. Bidhaa kama marashi ya chupa, mafuta na losheni za ngozi na mafuta ya nywele ni baadhi ya bidhaa unazoweza kuuza kwa faida nyumba ya buti ya gari lako.
8. Vito na bidhaa za kuvaa mikononi na shingoni
Bidhaa za kuvaa shingoni na mikononi ni biashara nyingine has a inayowagusa wanawake.
Bidhaa kama cheni za dhahabu,shaba,na madini mengine ya vito vya thamani yanahitajika na yanauzika kwa wingi. Bangili za mitindo tofauti kama plastiki,shaba,silva na madini mengine yanaweza kuwa biashara nzuri nyuma ya gari lako.
9. Mboga mboga na Viungo
Mboga mboga kama karoti,pipili hoho,vitunguu,nyanya chungu na bidhaa nyingine za bustanini kwako au hata kama utazinunua zinaweza kuuzika na kukuongezea kipato katika duka ndani ya gari lako.
10. Urembo wa Kucha na Mikono
Tumezungumzia zaidi bidhaa,lakini kuna huduma pia unazoweza kuzitoa katika gari lako. Urembo wa kucha kama kusawazisha kucha na kupaka rangi za kucha na vidole kama hina na piko ni mojawo ya huduma unazoweza kufanya katika gari lako.
11. Bidhaa za Biashara za Mtandao
Mojawapo ya biashara maarufu zenye faida siku hizi ni biashara ya
mtandao,ni biashara za kuuza bidhaa toka makampuni ambayo yanauza na
kusambaza bidhaa zake kwa kupitia mtu mmoja mmoja kwa njia ya mdomo.
Wasambazaji ni watu ambao wanatumia bidhaa hizo na wanapata malipo
kwa kuwashirikisha wengine na kuwasajili katika biashara. Baadhi ya
makampuni ya biashara ya mtandao ni kama yafuatayo:
Bidhaa hizi ni rahisi kuuza katika buti ya gari na ni rahisi kuwainesha na kuwashirikisha watu wengine kwa njia hii
[Soma: Biashara ya Trevo – Biashara ya Mtaji Mdogo Chini ya TSh. 500,000]
Mwisho
Japo biashara hizi si za kutegemea sana kama chanzo cha kwanza cha
kipato lakini zikifanywa vizuri zinaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa
kipato chako.
Wataalamu wa uchumi binafsi wanashauri kuwa na vyanzo zaidi ya kimoja
vya fedha ili kufanikiwa kifedha na biashara za kufanya katika buti ya
gari lako zinaweza zikasimama kama chanzo cha pili cha kipato.
Je wewe unafikiriaje? Kuna biashara nyingine katika mawazo yako
ambazo unaweza kufanya katika buti la gari lako? Shiriki nasi kuchangia
katika sanduku la maoni hapa chini.
Nakutakieni usomaji mwema na michango katika mada hii na muhimu zaidi
kufanya kwa vitendo angalau wazo mojawapo katika haya kumi. Tutaonana
tena katika mada nyingine
-----Prosper Muro----
No comments:
Post a Comment