SIFA ZA KUOMBA MKOPO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
JE, UTAOMBA MKOPO WA ELIMU YA JUU MWAKA HUU?•
1. Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania
2.Mwombaji a we ameomba kudahiliwa na Chuo Kikuu au Taasisi ya Elimu ya Juu inayotambuliwa na Serikali.
3.Asiwe mwanafunzi wa masomo ya jioni (Part time Student).
4.Asiwe na udhamini/ufadhili/msaada wa kifedha kutoka katika vyanzo vingine.
5.Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa mtandao (OLAMS).
6.Awe amefaulu mitihani ya mwisho wa mwaka (wanaoendelea na masomo) na matokeo yake kuwasilishwa Bodi ya Mikopo na chuo chake.
7.Awe amemaliza Kidato cha Sita au awe na sifa linganishi (kama Diploma n.k) ndani ya miaka mitatu (2015/2016–2017/2018).
8.Awe na umri usiozidi miaka 30 wakati wa kufanya maombi.
9.Waombaji ambao wazazi wao ni Wakurugenzi au Mameneja Waandamizi
katika Makampuni binafsi yanayotambuliwa na Mamlaka za Mapato na Usajili anatarajiwi kuomba;
10.Waombaji ambao wazazi wao ni viongozi wa umma au kisiasa ambao
wanatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hawatakiwi kuomba mkopo
Mwisho wa kuomba mkopo in Septemba 4, 2017
Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2017/18 unaopatikana kwenye tovuti:
www.heslb.go.tz
Ime Imetolewa na
:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
No comments:
Post a Comment