Header Ads

Aliyempigia debe Lowassa amsifia Rais Magufuli

Kama utakumbuka kipindi cha kampeni mastaa wengi wa Bongo Movie na Bongofleva walijitolea kutoa sapoti kwa wanasiasa ambao walikuwa katika harakati za kuomba ridhaa kwa wananchi kuongoza. Moja ya mastaa hao ni muigizaji Shamsa Ford ambaye alikua akimsapoti mgombea uraisi wa Chadema Edward Lowassa.
Hata hivyo msanii huyo hivi karibuni amefunguka na kumsifia Rais Magufuli kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya ikiwemo kuruhusu sera ya elimu bure kwa watanzania wote na kutengeneza misingi mizuri kwenye pesa.
...>>>”Mpaka sasa nampenda Lowassa na nipo Chadema lakini lazima kuwe na uzalendo kwanza. Tumefanya kampeni mwisho wa siku tumempata rais mmoja Magufuli. Kuna vitu vingi amevifanya rais na ninavipenda kama mtanzania, kwanza ni hii ya elimu bure, nimependa heshima aliyoiweka kwenye pesa” – Shamsa Ford

No comments:

Powered by Blogger.