Neymar amevunja rekodi ya dunia
Club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa imeweka rekodi ya dunia kwa kumsajili Neymar kwa mkataba wa miaka mitano lakini kubwa ni dau ambalo wamemsajili nalo hajawahi kusajiliwa nalo mchezaji yoyote, dau hilo ni mara ya mbili ya dau alilosajiliwa nalo Gareth Bale, Pogba na Cristiano Ronaldo.
Rekodi ya uhamisho wa Neymar inatabiriwa kuwa itadumu kwa muda mrefu, Neymar sasa anaungana na wabrazil wenzake Dani Alves na Lucas Moura wanaoitumikia PSG.
“PSG wamekuwa na mipango ambayo imenivutia kujiunga nao nimecheza misimu minne Ulaya sasa nafikiri huu ni wakati sahihi kupata changamoto mpya, kuanzia leo nitafanya kila liwezekanalo kusaidia wachezaji wenzangu na timu” >>> Neymar
No comments:
Post a Comment