MSANII MADEE AFUNGUKA DIAMONDI ALIVYOSAIDIA KOLABO YAKE NA TEKNO
Madee amesema haikuwa ngumu sana kumpata muibaji huyo kutoka Nigeria na
pia si yeye aliyeangaikia kolabo hiyo na hata pale Tekno alipoangalia
kazi zake hakuwa na pingamiza kuhusu kufanya hiyo ngoma.
“Nilimuelezea tu Babu Tale pamoja na Diamond, bwana naweza kufanya kazi
na Tekno?, wakasema inawezekana ngoja tumuambie nakumbuka alikuwa hapa
hapa Dar es Salaam, wakamwambia akasema nipeni kama lisaa limoja ili
nimuangalie huyu Madee,” Alisema Tecno
“Nadhani katika hilo lisaa limoja ndio akawa anamuangalia Madee ni nani,
amefanya nini na ana impact gani baada hapo akawajibu its ok tunaweza
kufanya lakini production nafanya mimi kwa sababu yeye ana studio,”
amesema.
Ameongeza kuwa, “kwa hiyo akapiga ile biti akafanya vocal akaja tena Dar
es Salaam kwenye mishe zake akatupatia ile biti pamoja na vocal
nikaweka vocal zangu akapewa tena alipoona ipo ok, ndio ikafanyika mixing
WCB,” amesema
No comments:
Post a Comment