Header Ads

Hayawi Sasa Yamekuwa || Yanga vs Simba Leo Agosti 23, 2017

HAYAWI Hayawi sasa yamekuwa, waliosema haifiki sasa imefika. Kwa lugha rahisi unaweza
kuzungumza hivyo baada ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambao wanakutana
katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam.
Baada ya tambo za muda mrefu za usajili kwa kila tambo na matokeo ya mechi za kirafiki,
maarufu kama kutesti mitambo, leo ni kazi kazi tu.
Ni miezi saba tangu miamba hiyo ikutane kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), ambako
Simba ilishinda mabao 2-1, licha ya kufungwa lakini Yanga iliweza kutetea
ubingwa wake wa VPL.
Ni msimu ambao mashabiki wa Simba waliandika historia kwa kung’oa viti katika mchezo wa
mzunguko wa kwanza, ambao timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Simba waling’oa viti, mshambuliaji wa Yanga,
Amissi Tambwe, alichafua hali ya hewa baada ya kufunga bao, ambalo alianza
kuunawa mpira kabla ya kutupia nyavuni.
Pia mchezo huo una kumbukumbu ya nahodha wa Simba, Jonas Mkude, kulimwa kadi
nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo, Martin Saanya wa Morogoro, ila kadi hiyo
ilikuja kufutwa na kamati baada ya kujiridhisha ilitolewa kimakosa.
Ila, hata katika mchezo wa Februari mwaka huu, Simba ilipata ushindi ikiwa pungufu mara
baada ya Abdi Banda kulimwa kadi nyekundu dakika ya 56.
Miamba hiyo leo inakutana katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii kila mmoja akihitaji
ushindi ili kulinda heshima yake na kuanza msimu wa 2017/18 kwa morali zaidi.
Simba wanashuka dimbani wakiwa ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC), wakati
Yanga wao ni mabingwa wa VPL msimu uliopita.
Hivyo basi, leo Afrika itasimama kwa dakika 90 kupisha pambano hilo la watani hao wa
jadi, Yanga na Simba, ambao ndio miamba ya soka la hapa nchini.
‘Dabi’ hiyo itapigwa kuanzia saa 11:00 jioni mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), kusogeza mbele baada ya awali kutangaza kuwa mchezo huo ungepigwa saa
10:00 alasiri, ili kutoa nafasi ya watu watakaokuwa kazini kuhudhuria.
Mchezo baina ya vigogo hawa ndio unatarajiwa kutoa taswira ya ubora wa vikosi vyao
msimu huu, kutokana kila mmoja kutoa tambo za kuwa ana timu bora kuliko
mwenzake na aina ya usajili ambao wamefanya.
Mechi hii ni kati ya ‘Dabi’ maarufu na kubwa
kabisa Afrika na inatajwa kuwa ni ya tatu baada ya Al Ahly  Vs Zamalek za Misri ambayo inatajwa namba moja halafu inafuata ‘Soweto Derby’ kati ya Orlando Pirates Vs Keizer Chiefs za
Afrika Kusini na hii ya Yanga na Simba.
NIYONZIMA, AJIB GUMZO
Usajili wa Ibrahim Ajib kwenda Yanga na Haruna Niyonzima kujiunga na Simba, kumeongeza
chachu katika mechi ya leo inayofuatiliwa na watu wengi.
Lakini ukiacha hao, pia ujio wa Emmanuel Okwi wa Simba, ambaye ana ngekewa ya kuifunga
Yanga, unatia homa katika kikosi cha Wana Jangwani hao kwenye mtanange wa leo.
Ila, kwa Yanga wana kiu ya kuona vitu vya Mkongo, Kamba Tshishimbi, ambaye amesajiliwa
kuziba pengo la Niyonzima aliyetimkia Simba, hivyo leo anatakiwa kudhihirisha
ubora wake.
Wachezaji hawa ndio waliteka soko la usajili kwa muda mrefu, lakini toka walipojiunga
kumekuwa na maneno mengi kutoka kwa mashabiki, hivyo wanataka majibu yao
uwanjani.
Kiuhalisia wachezaji hawa wanaweza kucheza kwa presha kubwa mno kutokana na kiu ya
kuhitaji kuonyesha umwamba katika mchezo huo muhimu.
BOCCO, KAPOMBE, TSHABALALA, CHIRWA NJE
Kuelekea katika mchezo huo, Simba itawakosa mshambuliaji wake John Bocco ‘Adebayor’,
beki Shomari Kapombe, huku Nahodha wao Msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’
akiwa kwenye hati hati baada ya kupata majeraha katika mchezo wa kirafiki
waliocheza dhidi ya Gulioni kwenye Uwanja wa Amaan.

No comments:

Powered by Blogger.