Header Ads

Afande Sele Baada ya kutajwa kwenye Zilipendwa ya WCB-"Huu Msiba Hauwahusu"

Siku moja baada ya team WCB ikiongozwa na Diamond Platnumz kuachia video ya wimbo wao wa kundi ‘Zilipenda’ kisha kuibua maswali kwa baadhi ya mashabiki kutokana na maudhui ya wimbo huo kwa kuwataja baadhi ya mastaa wa zamani, mmoja wa aliyetajwa ambaye ni Afande Sele kafunguka.

Kupitia Instagram yake, Afande Sele aliandika ujumbe ambao unaashiria kutokasirika wala kuchukizwa na kitendo cha kutajwa kwenye ‘ZILIPENDWA’ na kuonesha kufurahia jambo hilo mbali na wengine huku akiwaambia walioupokea vibaya msiba hauwahusu.
Afande Sele aliandika>>>Sana mdogo wangu nyakati zinabadilika Huu muda wa akina Damian sio nyakati za Burning Spear au Bob Marley , ndio maana nikawa Muhenga, wamuache Dogo afanye kazi zake #safiplatnumdiamond @Regrann from @rhymesselassie – Simba wa Morogoro nae zilipendwa … Simba wa madale/tandale kanichekesha. Safi this is music , #burudani, utani kwa mhenga. Nawashangaa linaowatoka povu wakati msiba hauwahusu.

No comments:

Powered by Blogger.