Pesa za usajili wa Neymar kuzibomoa Chelsea,Liverpool na Tottenham
Neymar Dos Santos anaonekana anaondoka Barcelona, siku za
karibuni kumekuwa na mambo mengi yanayomhusu nyota huyo yanayoashiria
mwisho wake wa kukipiga Nou Camp umefika.
Ugomvi wake wa jana na mlinzi Nelson Semedo umezifanya tetesi za yeye
kuondoka Barcelona kuzidi kukua huku Barcelona wenyewe nao wanaonekana
wako tayari kumuachia mshambuliaji huyo aondoke.
Tayari Barca wameshaanza kutafuta mtu atakayeziba nafasi ya Neymar na
kati ya vigezo wamekuwa wakiangalia sio tu ubora wa mchezaji husika
lakini pia umri wa wachezaji wanaowataka.
Phellipe Coutinho ndilo jina ambalo kwa sasa lipo katika makaratasi
ya kamati ya usajili wa Barcelona, Coutinho anaonekana kuhitajika zaidi
katika klabu ya Barcelona kuliko mchezaji mwingine yoyote.
Coutinho sii tu kwamba anaweza kuchukua nafasi ya Neymar lakini kwa
muda mrefu Barcelona wanamfuatilia Neymar wakiamini anaweza kuchukua pia
nafasi ya Andre Iniesta ambaye umri umeanza kumpa mkono.
Chelsea nao hawako salama na pesa za Neymar, wiki hii kumeibuka taarifa ya kwamba Barcelona wanajaribu kumshawishi Eden Hazard kuachana na mpango wa kwenda Liverpool na ajiunge nao.
Tottenham wanafurahia sana kwa sasa huduma ya Delle Ali kiungo ambaye
amekuwa gumzo sana duniani kiasi cha kuzivutia klabu kubwa nyingi
duniani ikiwemo Real Madrid,Chelsea na Manchester United.
Barca nao wameingia kwenye mpambano wa Ali na inasemekana kwamba wako
tayari kutoa £75m kumnunua, usajili ambao Tottenham hawako tayari hata
kuuzungumzia kwani hawataki hata kidogo kusikia habari za Ali kuondoka.
No comments:
Post a Comment