Mkude amevuliwa unahodha Simba
Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa
kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu
ya Simba,akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji
mwandamizi kwenye kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika
kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua
Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu
huu,Mohammed Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha
wasaidizi wa timu hiyo.
Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji
wake mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote
alipokuwa Nahodha wa Timu.
Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda
vema huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa habari Simba SC
*SIMBA NGUVU MOJA*
No comments:
Post a Comment