Header Ads

Oparesheni zaidi ya 10, Millen Magese apata mtoto

 
Millen Magese, Kuna kipindi alikata tamaa mpaka akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada ya kufanyiwa  oparesheni zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo, aliambiwa moja ya tiba ya tatizo hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa kizungu, ni kuzaa.
Baada ya mateso yote usiku na mchana pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye matibabu South Africa na Marekani, leo hii Millen anayofuraha kuitangaza habari njema kuwa amefanikiwa kupata mtoto wa kiume July 13 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo Michael Magese.

No comments:

Powered by Blogger.