Marehemu Michael Jackson kumlipa mtayarishaji wa albamu ya ‘Thriller’
Mahakama nchini Marekeani, imeamuru mtayarishaji wa muziki Quincy Jones, aliyetengeneza albamu kama ‘Thriller,’Of The Wall’ na ‘Bad’ alipwe kiasi cha Bilioni 20.7.
Mtayarishaji huyo atalipwa pesa hiyo na kampuni ya Michael Jackson baada ya kushinda kesi ya madai iliyofunguliwa mnamo mwaka 2013 kwa kutomshirikisha katika malipo ya remix ya nyimbo alizotengeneza.
Remix ya nyimbo hizo zilitengenezwa baada ya kifo cha mkali huyo wa Pop dunia ndipo kampuni yake haikufanya mazungumzo na Jones hali iliyopelekea kufungua kesi na kudai kiasi cha dola Milioni 30, lakini kampuni ikasema kuwa Jones anaidai dola za Marekani 392,00.
Kwa mujibu wa mtandao wa AP umeeleza kuwa mtayarishaji huyo alidanganywa wakati anakula kiapo juu kuwa atapatiwa fedha nyingi. Pia mtandao wa Billboard ulinukuu kuwa Jones alisema kuwa hukumu hiyo ni ushindi wa sanaa.
Na Laila Sued
No comments:
Post a Comment