Majambazi wawili wameuawa na Polisi Kibiti…risasi zarindima
Kupitia Taarifa ya Habari kwenye
Televisheni za Tanzania leo July 20, 2017 zipo taarifa nyingi
zimeripotiwa na moja kubwa ni kuhusu mapambano ya Polisi dhidi ya watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi katika operesheni maalum Kibiti, Pwani.
Taarifa hiyo ambayo imerushwa na Kituo cha Channel 10 ambapo wakati
wa zoezi la kuwasaka wahalifu likiendelea Kibiti leo imeripotiwa kuwa
Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa
wahalifu hao.
Mkuu wa Operation hiyo Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabaas
amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Utende lililopo Kata ya
Ukwiriri Wilayani Rufiji baada ya Polisi kuwatilia shaka watu watano na
walipowafuatilia walikimbia na kuwashabulia Askari kwa risasi na katika
majibizano Askari walifanikiwa kuwajeruhi wawili ambao walifariki njiani
wakati wanapelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili.
>>>”Baada ya
kuwasimamisha watu wale hawakusimama walikimbia na kisha kufyatua risasi
hewani kuelekea walipokuwa Askari. Askari walijibu mapigo na kufanikiwa
kuwajeruhi watuhumiwa wawili kati ya wale watano na wakati wanapelekwa
Hospitali walipoteza maisha.” – Liberatus Sabaas.
No comments:
Post a Comment