JAY Z ameshindwa kuvunja rekodi hii ya DJ Khaled kwenye Billboard
Pamoja na kufanikiwa kutunukiwa heshima ya mauzo makubwa ya Platinum kabla ya wiki moja, bado albam mpya ya rapa mkongwe JAY-Z (4:44) haijafanikiwa kuingia kwenye rekodi za mauzo makubwa ya albam za mastaa wa muziki duniani Billboard charts.
Kama ilivyokuwa kwa mshkaji wake Kanye West ambaye kwasasa hawako poa kama zamani, albam yake ya The Life of Pablo nayo haikufanikiwa kuingia kwenye chart za Billboard na zote zinaelezwa kusababishwa na albam hizo kuachiwa kwanza kwenye mtandao wa TIDAL ambao taarifa zake za mauzo hazitumiki taasisi ya utafiti wa mauzo ya Nielsen Music.
Hata hivyo, ndani ya masaa 24 tangu kuachiwa kwa albam ya JAY Z kwenye iTunes Ijumaa ya wiki iliyopita imefanikiwa kushika number #1 kwenye nchi 38 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani, Canada, Australia, Mexico, Denmark, Ireland, Norway, Switzerland, Russia, Sweden, South Africa, Finland, Poland, Malaysia, India, Panama, Sri Lanka, Anguilla, Antigua, Bahamas, Barbados, Bermuda, Botswana, Ghana, Indonesia, Israel, Kenya, Nigeria, Uganda, Trinidad, Tobago, Saudi Arabia, Mozambique, Lebanon, Saudi Arabia, Namibia na Zimbabwe.
Ukipita kwenye chart za Billboard 200, albam ya DJ Khaled “Grateful” bado inashika nafasi ya kwanza kama albam bora kwa wiki ya pili mfululizo ikiwa imeuza nakala 70,000 ndani ya wiki hii pekee. Kwa mujibu wa Billboard hadi kufikisha kiasi hiko ngoma za albam ya Grateful zimesikilizwa mara milioni 63.4 ndani ya wiki hii.
No comments:
Post a Comment