Jamal Malinzi na wenzake watia huruma, Mahakamani leo
Na Muro TV (Mr Muro)
Leo July 3, 2017 Mahakama ya Hakimu Mazi Kisutu imetupilia
mbali maombi ya upande wa utetezi kutaka Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake kupatiwa dhamana.
Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga walifikishwa Mahakamani leo wakikabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha Dola za Marekani, 375,418.
Kutokana na kukataliwa maombi hayo kesi ya Malinzi na wenzake iliahirishwa hadi July 17, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
Aidha, Mahakama hiyo imewaonya Mawakili wa upande wa utetezi
ikiwataka waache ubabaishaji wa kuizungumzia kesi hiyo kwenye vyombo vya
habari badala yake wawasilishe hoja zao mbele ya Mahakama.
No comments:
Post a Comment