Header Ads

Cristiano Ronaldo Mahakamani kesho kwa ukwepaji wa kodi

 
Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, kesho Jumatatu ya July 31 2017 atapandishwa mahakamani Hispania kuanza kusikiliza kesi yake ya tuhuma za ukwepaji kodi.
Ronaldo atapandishwa kizimbani akiwa bado hajaanza mazoezi ya maandalizi ya msimu akiwa na Real Madrid,  kesi inayomkabili Ronaldo ni ukwepaji kodi mwaka 2010 wakati wa mauzo ya haki ya picha zake.
Ronaldo atapandishwa mahakamani kujibu tuhuma za ukwepaji kodi wa euro milioni 14.7, kama utakuwa unakumbuka Ronaldo anaingia katika skendo ya ukwepaji kodi kama ilivyokuwa kwa mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona mwaka uliopita.

No comments:

Powered by Blogger.