Waonywa kuigeuza Tanzania Dampo la bidhaa zisizo na ubora
Wauzaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na mawakala wa forodha Kanda ya
Kaskazini, wameonywa kuacha kuigeuza Tanzania kuwa dampo la bidhaa
zisizo za ubora.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro ametoa onyo hilo leo
alipofungua semina ya wafanyabiashara na mawakala hao, iliyoandaliwa na
Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Daqarro amesema wauzaji wa bidhaa kutoka nje na mawakala wa forodha
wana wajibu wa kuhakikisha wanafuata utaratibu wa TBS kuhakiki ubora wa
bidhaa kabla ya kuletwa nchini
Tanzania si dampo la bidhaa zisizo na ubora, hivyo ni wajibu wenu,
kuwasiliana na kampuni za uhakiki wa bidhaa zilizoteuliwa na TBS nje ya
nchi ili kuhakikisha ubora wa bidhaa kabla ya kuzileta nchini," amesema
Ridhiwani Ramadhani, ambaye ni kaimu mkurugenzi wa udhibiti wa ubora wa
bidhaa na mkuu wa ukaguzi wa TBS, amesema ukaguzi wa bidhaa unatakiwa
kufanyika nje ya nchi ili kuondoa tatizo la bidhaa zisizo na ubora
kuingia nchini
Amewataka wauzaji wa bidhaa na mawakala wa forodha kuzitumia kampuni za
ukaguzi zilizoteuliwa na TBS kuhakikisha hawapati hasara kwa kuingiza
nchini bidhaa sisizo na ubora.
Ramadhani amesema TBS itaendelea kuongeza ukaguzi na udhibiti wa bidhaa zisizo na ubora kuingia kupitia mipaka yote nchini.
Mfanyabiashara, Rajan Razak ameitaka TBS kuwatangaza kwenye vyombo vya
habari mara kwa mara mawakala wa ukaguzi wa bidhaa nje ya nchi na sehemu
wanakopatikana ili kuwaondolea tatizo la kutokaguliwa bidhaa zao kabla
ya kuingia nchini
Muro Tv Ipo Play Store…Download HAPA ,Tuwe tunakutumia habari kwa haraka zaidi,kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba:0768786851, whatsapp:0768786851

No comments:
Post a Comment