WAKILI AELEZA SHERIA KUHUSU KUFUKULIWA KABURI LA IVAN
MuroTv
Wakili aeleza sheria kuhusu kufukuliwa Kaburi la Ivan

Kufuatia ombi hilo la Mahakama ya Uganda leo June 3, 2017. Wakili wa kujitegemea na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Tanzania Jebra Kambole ambaye anafafanua zaidi…
“Nilichokiona kwenye shauri ambalo limefunguliwa Uganda ni maombi ambayo yamefikishwa Mahakamani na Mahakama ndiyo ina jukumu la kuyatafsiri yale maombi. Kwa hiyo siyo amri ya Mahakama moja kwa moja.
“Ni maombi ambayo yamepelekwa chini ya kifungu namba 42, kifungu pia cha 17, kifungu kidogo cha kwanza (a) na (i) ya Katiba ya Uganda ya mwaka 1965, lakini pia kifungu cha 50 cha Katiba ya Uganda.
“Kimsingi, vifungu hivyo ambavyo nimevitaja hapo awali vya Katiba ya Uganda ni vifungu ambavyo moja kwa moja vinatoa wajibu kwa kila raia kuheshimu alama za Taifa ikiwemo pamoja na pesa ya nchi.” – Jebra Kambole.
SIKILIZA NYIMBO MPYA YA KING DAVY-KWA MUDA
No comments:
Post a Comment