Taifa Stars imeshindwa kupata ushindi vs Angola COSAFA 2017
Tanzania leo imecheza dhidi ya Angola wakati Malawi ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania kwa magoli 2-0, imecheza dhidi ya Mauritius ambayo pia ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Angola huku staa wa Tanzania Mzamiru Yassin akiibuka mchezaji bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola.
Katika michezo ya leo Tanzania ililazimishwa sare na Angola huku pia Malawi na Mauritius zimemaliza dakika 90 bila kufungana. Kwa matokeo hayo Tanzania bado inaendelea kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne sawa na Angola ila anaongoza kwa tofauti ya magoli. Katika michuano hii timu vinara wa makundi ndio watafuzu kucheza robo fainali.
No comments:
Post a Comment