Header Ads

SIKU YA MAZINGIRA KITAIFA KUFANYIKA MARA, JUNE 05, 2017

MuroTv

"Tunza mazingira kufikia malengo ya uchumi wa viwanda" 

 01 Juni 2017

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akiotesha mti ikiwa ni ishara ya utunzaji wa mazingira
MKUU wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva ameitaka jamii kutunza na kuhifadhi mazingira ili kufanikisha nchi kufikia uchumi wa viwanda.
Lyaniva ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua wiki ya Mazingira katika Wilaya hiyo ambapo kitaifa maadhimisho ya wiki ya mazingira yanatarajiwa kufanyika Mkoani Mara Juni tano mwaka huu.
Amesema ni wajibu wa kila mwananchi kutunza na kuhifadhi mazingira kwani bila mazingira rafiki hawataweza kufikia malengo ya dhana ya uchumi wa viwanda na kutasababisha madhara makubwa ya uharibifu wa mazingira.
Lyaniva pia amewaelekeza wananchi wa Wilaya hiyo kuhakikisha kila mmoja anashiriki katika kupanda mti katika eneo lake na amewataka maofisa mazingira kuhakikisha wanapita katika maeneo yote ya Wilaya hiyo ili kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika shughuli ya upandaji wa miti.

No comments:

Powered by Blogger.