Serikali Imetangaza rasmi, nafasi za kazi 15,000 katika sekta mbali mbali za Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
amesema tayari serikali imetoa kibali cha ajira 15,000 kwa ajili ya
kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliofutwa kazi baada ya
waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi katika kada mbalimbali.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati aliyetaka
kujua mpango wa serikali kuhusu kujaza nafasi zilizoachwa wazi na
watumishi wa umma walioacha kazi kufuatia agizo la Rais Magufuli
alilolitoa mapema Mei mwaka huu. Waziri Kairuki alisema kuwa ni kweli baada ya watumishi hao
kuondoka katika vituo vyao vya kazi, sehemu mbalimbali zilikumbwa na
uhaba wa watumishi na hivyo kupelekea kuzorota kwa utoaji wa huduma.
Lakini ili kukabailiana na hilo, hivi karibuni serikali imetoa kibali
cha kuajiri watumishi wapya kujaza nafasi hizo. Mei mwanzoni Rais Magufuli aliagiza hadi Mei 15 mwaka huu
watumishi wote waliotajwa katika orodha ya wenye vyeti vya kughushi
waondoke mara moja la si hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
SIKILIZA WIMBO MZURI UNAOPINGA ULAWITI KWA WATOTO
Song: Anza SaSa
Artist: Fresh Andy ft Stino & K-Sam
FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
CLICK HAPA ☛OPEN FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM
No comments:
Post a Comment