RC Gambo afanya mazungumzo na balozi wa Ufaransa kuboresha utalii mkoani Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiwa Ufaransa, amefanya
mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Samwel W
Shelukindo. Ufaransa ni moja ya zinazoleta watalii wengi nchini
Tanzania. Pamoja na mambo mwingine wamejadiliana Yafuatayo:-
1. Mambo ya Msingi ya kufanya ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa kuja Arusha
2. Kupata wawekezaji kutoka Ufaransa kuja Arusha (Fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Arusha )
3. Kuanzisha tukio la kimataifa la kutangaza utalii mkoani Arusha kila mwaka
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo yupo katika ziara ya mafunzo
nchini Ufaransa pamoja na mafunzo hayo amekua akiutangaza mkoa wa Arusha
kama kitovu cha utalii nchini Tanzania. FOLLOW NA LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK HAPA CHINI
CLICK HAPA ☛OPEN FOLLOW ACCOUNT YANGU YA INSTAGRAM
No comments:
Post a Comment