PICHA: MAZISHI YA SHABIKI MAARUFU WA YANGA, “ALLY YANGA’
Mwili
wa Shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed ali maarufu kwa jina
la Ally Yanga aliyefariki dunia juzi katika ajali ya gari aina ya Rav4
eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umezikwa leo
katika makaburi ya Nguzo Nane mjini Shinyanga.
Mbali na kuwa mshabiki wa Yanga Ally Yanga pia alikuwa mkereketwa wa
Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya
Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na siyo
kwamba alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.
Ally alizaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya
watoto sita, kabla ya umauti wake alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es
Salaam.
Picha za Ally Yanga enzi za uhai wake
Mwili wa marehemu Ally Yanga ukiwa umebebwa kwa ajili ya mazishi katika
makaburi ya Nguzo Nane Mjini Shinyanga leo alhamis June 22,2017.
Mwili wa Marehemu Ally Yanga ukizikwa kwenye makaburi ya Nguzo Nane mjini Shinyanga
Awali kabla ya mazishi,Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiombea mwili wa marehemu Ally Yanga
Naibu katibu mkuu CCM bara Rodrick Mpogolo akitoa salamu za pole kwa
niaba ya Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais John Pombe Magufuli
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali
Naibu kartbu mkuu CCM bara Rodrick Mpogolo akisaini kitabu cha
rambirambi nyumbani kwa Marehemu Ally Yanga Stendi ya Mabasi ya wilaya
mjini Shinyanga
Mkuu wa Wilaya Josephine Matiro( wa tatu kutoka kulia) , akifuatiwa na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa msibani
Wananchi,wapenzi wa mpira wa miguu na viongozi wa serikali ,wabunge
wakiwa kwenye maombolezo nyumbani kwao na marehemu Ally Yanga mjini
Shinyanga

No comments:
Post a Comment