MAPENZI : Mambo usiyopaswa kuwasirikisha Marafiki kuhusu mapenzi yako
1. MASWALA YA KIFEDHA.
Si vyema kuwashirikisha rafiki zako au ndugu zako kuhusu mipango yenu ya
kifedha. Ikiwa mnamipango yoyote ya uwekaji akiba au mkopo mmekopa si
vyema kuwashirikisha watu kwani wakati mwengine huweza kusababisha
mpenzi wako kudharauliwa na marafiki au ndugu zako.
2. KUTOA HISTORIA YANYUMA YA MWENZI WAKO
Kila mtu upitia yakwake kwenye maisha, wengine walisalitiwa, walifanya
matukio ya ajabu huko nyuma kabla ya kukutana na wewe. Sasa si jambo la
busara kukaa na marafiki zako au ndugu zako na kuanza kuzungumzia maisha
ya nyuma ambayo mpenzi wako alikua anayaishi kabla ya kukutana na wewe,
mpaka yeye amekushirikisha basi jua wazi kabisa amekuamini kitendo cha
kutoa siri zake si jambo jema.
3.MATATIZO YA NDUGU WA MPENZI WAKO.
Kila nyumba inamatatizo yake kwakua kila mtu anatabia yake. Ikiwa
imetokea umeghafilika na tabia za shemeji yako au wifi yako ni vyema
umwambie kaka au dada yako kuhusu ilo kuliko kutoka kwenda kuwaambia
watu wa pembeni. Ikitokea mpenzi wako amefahamu hilo basi utamkwaza sana
na hatokuwa na imani na wewe.
4. MATATIZO YA NDANI.
Nyumba inaficha mambo mengi sana na kuwa kwenye mahusiano kunahitaji
uvumilivu mkubwa. Migogoro haiepukiki ndani ya nyumba na japo si vyema
kuiendekeza. Ikiwa kuna matatizo ndani ya nyumba komaa nayo usipende
kuwashirikisha marafiki au ndugu zako. ukiwa kama mpenzi unanafasi kubwa
sana ya kutatua matatizo ya ndani kwako kuliko kutoka na kuyasema nje.
5. MPENZI WAKO AKIWA NA KASORO FULANI
Kila mtu anaudhaifu wake. Mfano kuna wanaume hawawezi kwenda mizunguko
miwili na wapenzi wao, kuna wengin wanauume mdogo na kuna wanawake
wanatoa maji au harufu mbaya kwenye uke, matatizo kama haya si vyema
kuwaambia ndugu au rafiki zako kwa maana utatengeneza mazingira ya
mpenzi wako kudhalilika pasipo wewe kujua.
No comments:
Post a Comment