CHADEMA wameeleza kuhusu Lowassa kuitwa kwenye mahojiano na DCI
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward
Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)
kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kesho Jumanne, saa 4
asubuhi kwa ajili ya mahojiano. Taarifa iliyotolewa na CHADEMA imesema
kuwa hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo
yatahusu nini hasa.
CHADEMA wameeleza kuwa taarifa za awali
zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Lowassa
alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari
katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kwenye vyombo vya habari leo Lowassa
ameripotiwa akimtaka Rais Magufuli kuwaachia huru mashehe wa uamsho
ambao inadaiwa wanashikiliwa kwa miaka minne sasa.
No comments:
Post a Comment