KIVAZI CHA MREMBO KAJALA CHAZUA GUMZO UKUMBINI
Staa mtata katika kinu cha ‘kutwangia’ filamu Bongo, Kajala Masanja.
Staa
mtata katika kinu cha ‘kutwangia’ filamu Bongo, Kajala Masanja, ambaye
kama utasumbuka kumtambua kwa jina hilo, mtaje kwa ufupi wa Mama Paula,
amerudi tena na awamu hii amezua gumzo kwa kuteka akili za watu, hususan
wanaume wakware, kufutia kutinga kinguo kifupi ‘mini-sketi’ ukumbuni,
hali iliyoibua viulizo na maswali kibao, teremsha macho hapa chini.
Ilikuwa
Jumatatu, siku ya Eid-mosi ndani ya Ukumbi wa King Somolon uliopo
Namanga jijini Dar, ambako pamoja na shamrashamra zingine, kulikuwa na
shoo ya kukatika shoka na mpini kubaki, ikiwakusanya wasanii wa
vichekesho kutoka nchi za Tanzania, Kenya na Uganda iliyoitwa jina la
Eid-Comedy Gala, huku Kajala akiwa miongoni mwa wahudhuriaji wa mtanange
huo.
Awali,
‘kiranja’ wa mtandao huu namba moja kwa habari za mastaa Bongo,
aliyekuwa ameweka kambi nje kidogo ya ukumbi huo alimshuhudia msanii
huyo aliyekuwa kimya kwa muda mrefu sasa, akiingia ndani sanjari na
kampani na watu wake wa karibu akiwemo mwanaye Paula ambaye akikaa mbali
na mama yake, huku Kajala akichagua viti vya mbele.
Kajala na mwanaye Paula
Miguno,
mishangao, viulizo na maswali vilianza kurindima chini kwa chini
ukumbini humo, baada ya Kajala kukaa na ‘kisketi’ chake kupanda juu
zaidi kutokana na ufupi wake, hivyo kuacha wazi sehemu kubwa ya mapaja
yake huku akijaribu kutumia mkoba wake kuzibaziba hali iliyolazimisha
macho ya wengi kuweka kambi juu ya eneo hilo nyeti la mwili wake.
Paula katika pozi
“Aaaah,
jamani hii sasa ni too much, huyu msanii mbona habadiliki tu? Hivi
haoni kama umri wake umekwenda na ukitazama mwanaye ameshakuwa binti
mkubwa, hadi avae mavazi yanayoacha wazi sehemu nyeti kama mapaja? Aibu
gani hii jamani? Ona sasa watu wanavyomshangaa!” walisikika baadhi ya
watu waliokuwa wamekaa karibu na mwandishi wetu, wakijadili uvaaji huo
wa kihasara wa msanii huyo.
Kwa
upande wake, licha ya macho ya wengi kumtazama mfululizo, Kajala
hakuonekana kujali hali hiyo na badala yake alijikita zaidi kufuatilia
vichekesho vilivyokuwa vikiangushwa jukwaani na wasanii hao ‘alwatani’
katika eneo la uchekeshaji na mwandishi wetu alimkaribia na kumuuliza
kuhusu kinguo chake ambapo alipotezea kiaina kama maswali ya mwandishi
hayakumhusu yeye.
No comments:
Post a Comment