Header Ads

Hospitali ya Sengerema yakabiliwa na upungufu wa chupa za damu 350

MuroTV

MATUKIO

Hospitali ya Sengerema yakabiliwa na upungufu wa chupa za damu 350

Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza inakabiliwa na upungufu wa damu kwa kiasi kikubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mtalaamu wa Maabara  Wilayani Sengerema, Alex Lweyemamu ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu salama duniani ambapo amewaomba wananchi kujitokeza na kujitolea    kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye uhitaji wa  damu.
Lweyemamu amesema kuwa kwa wastani kwa mwezi mmoja hospitali hiyo inatakiwa ipate chupa za damu salama 350 lakini inashindwa kufikia kiwango hicho kutokana na mwitikio hafifu wa wananchi kujitolea damu kwani tangu kampeni ya uchangiaji damu ianze Juni mosi mwaka huu  hadi  June  14  ni jumla ya chupa 89 pekee zimechangiwa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliowahi kuchangia damu salama wameitaka jamii kuwa na mwamuko wa kusaidia   watu wenye uhitaji wa damu huku wengine  wakiiomba serikali kutoa elimu juu ya umhimu wa uchangiaji damu.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Misheni Wilaya ya Sengerema, Devis Lusobangija ameiomba jamii kujitokeza kuchangia damu ili kuwaokoa watu wanaokabiliwa na upungufu wa damu.

No comments:

Powered by Blogger.