DC BYAKANWA ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOWE.
MuroTV
MATUKIO
DC BYAKANWA ASIMAMIA ZOEZI LA UONDOSHAJI WA MIUNDO MBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA SHAMBA LA KILIMO CHA KISASA LA MBOWE.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius
Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai katika lango
la kuingilia katika shamba la Kilimo cha Kisasa la Mboga Mboga la
Kilimanjaro Vegees Ltd lililopo Nshara Machame.
Mkuu wa wilaya ya Hai,akiwaongoza
wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya Hai ,pamoja na askari
Mgambo wakiingia katika shamba la Kilimo cha Kisasa cha Mboga mboga la
Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman
Mbowe.
Shamba la Kilimo cha Kisasa,(Green House) lililopo Nshara Machame wilaya ya Hai la Kilimanjaro Vegees Ltd .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa
akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai,wakiwa katika moja
ya shamba hilo pamoja na asakari polisi wenye silaha wakiondoa miundo
mbinu ya umwagiliaji pamoja na unyunyiziaji wa dawa .
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa
akizungumza katika eneo hilo wakati zoezi la kuondoa miundo mbinu
katika eneo hilo ikiendelea.Zoezi hilo limefanyika kwa kile kinachodaiwa
shughuli za kilimo kufanyika kando ya mto kinyume cha sheria.
Sehemu ya Shamba la Strawberry kabla ya kuondolewa miundo mbinu.
Askari Mgambo wakiondoa miundo mbinu ya
umwailiaji katika shamba la Kilimoa cha Kisasa la Kilimanjaro Vegees
Ltd linalomilikiwa na Mbunge wajimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Mipira maalumu iliyokuwa ikitumika katika umwagiliaji ikiwa imekatwa katwa .
Asakari Mgambo wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akifuatilia zoezi la uondoshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji katika shamba hilo.
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius
Byakanwa akisaidia katika uondoshaji wa miondo mbinu katika shamba la
kisasa la Kilimanjaro Vegees Ltd linalomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la
Hai,Freeman Mbowe.
Askari Mgambo wa kikata mipira kwa panga .
Zao la Strawberry ni moja wapo ya mazao yanyolimwa kisasa katika shmaba hilo.
Sehemu ya Mazao ambayo tayari yameanza kukomaa katika shamba hilo.
Kilimo cha kisasa cha zao la Nyanya pia kimekuwa kikifanyika katika shamba hilo.
Baadhi ya Green House zikiwa zimeondolewa wavu maalumu wa kuzuia wadudu kuingia ndani.

No comments:
Post a Comment