DC KASESELA AKESHA MGODINI NYAKAVANGALA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI
MuroTV
MATUKIO
DC KASESELA AKESHA MGODINI NYAKAVANGALA KUOKOA MAITI YA MCHIMBAJI
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika mgodi wa
nyakavangala uliopo katika Kata ya malengamakali Mkoani Iringa wakati wa
Juhudi za kuuokoa mwili wa marehemu viskadi nyenza katika shimo
alilosimama Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akisaiadiana na wachimbaji
madini katika mgodi wa nyakavangala ili kuokoa mwili wa marehemu Nyenza
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alipokuwa akiwasili katika
mgodi wa nyakavangala uliopo Kata ya malengamakali Mkoani Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alilazimika kufanya kazi ya
uokoaji wa maiti ya mchimbaji madini katika mgodi wa Nyakavangala bwana
Vaspa Nyenza mkazi wa Itengulinyi Kata ya Ifunda wilaya ya Iringa kwa
takribani masaa kumi na nane
Kasesela alisema kuwa alianza kazi hiyo majira ya saa mbili asubuhi
alipowasili katika mgodi huyo wa Nyakavangala lakini yeye,waandishi wa
habari na viongozi wengine wa wilaya ya Iringa walijitahidi kuokoa mwili
wa marehemu hadi majira ya saa sita usiku lakini zoezi hilo lilikuwa
likiendelea
“Hadi saizi tumepiga dua zote lakini hali ngumu sijui nini kinaendelea
katika hili shimo maana waokoaji kila wakiukaribia mwili wa marehemu
miamba laini inavungika na kujaza udongo ndani ya shimo ndio maana
mmeniona naangaika na ndugu wa marehemu kujaribu kusali huku na kule
lakini hali ni ngumu hadi muda huu wa saa tano usiku”alisema Kasesela
Aidha Kasesela aliwataka ndugu wa marehemu na viongozi mbalimbali kuwa
na subila wakati wanalishugulikia swala la kuokoa mwili wa mpendwa wao
kwa kuwa wameshaukaria mahali ulipo.
“Ungalia tayari kichwa na kiwiliwili vimeshaonekana kwa hiyo
tumebakiza sehemu ndogo tu naombeni tuwe wavumilivu kwa kuwa tuvumilia
toka siku ya jumapili hadi usiku huu basi tuungane kumuombea mwenzetu
ili tutoe mwili wake ukiwa salama” alisema Kasesela
Haya yamemkuta mchimbaji mwenzenu hivyo nawataka kuwa makini wakati wa
uchimbaji wa madini katika mgodi huu wa nyakavangala la sivyo mgodi huu
utafungwa sio muda.
Lakini mwili wa Vaspa Nyenza umepatikana saa 7 na dakika 50 usiku na msafara kuelekea mortuary umeanza na Mazishi kufanyika Kijiji cha Itengulinyi Ifunda kesho asubuhi kuanzia saa 3 au 4 hivi
Lakini mwili wa Vaspa Nyenza umepatikana saa 7 na dakika 50 usiku na msafara kuelekea mortuary umeanza na Mazishi kufanyika Kijiji cha Itengulinyi Ifunda kesho asubuhi kuanzia saa 3 au 4 hivi
Kwa upande wake Chief inspector Mayunga Ngele aliwataka wachimbaji
wote kutochimba tena kwenye mashimo yaliyozuiliwa ili kuepusha ajali
mbalimbali hapo mgodini kwa kuwa hata huyo marehemu na wenzake
walishakatwa kuchimba katika shimo hilo ambalo lilikuwa kwenye hali
mbaya ya kuanguka.
“Tamaa ndio zimemponza huyu marehemu maana tuliwakataza lakini
mwenyewe waliingia kinyemela kwa lengo la kwenda kuchimba kwa wizi
kwenye shimo lilokataliwa ndio maana yamewakuta hayo kama wangekuwa
wameusikia ushauri wetu basi tusingefika hapa tulipo usiku huu “alisema
inspector Ngele
Naye Thomas masuka mmiliki wa mgodi wa Nyakavangala alimshukuru mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa jitihada zake za kuhakikisha
kila kitu kianda kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali na
kuahidi kuwa gharama za kuuokoa mwili hadi kuufikisha kwako ni kwake na
ndugu hawatalipia pesa yoyote ile.
“Kuanzia kutokea kwa kifo chake,uokoaji na kuusafirisha mwili wa
marehemu huyu gharama zote nitazilipa mimi kama mmiliki wa mgodi huu kwa
mujibu wa sheria za madini hata angekuwa Mwananchi wa kigoma,Mwanza,
Mbeya, Bukoba na sehemu yoyote ile ndani ya Tanzania basi ni wajibu
wangu kuhakikisha mwili wa marehemu unafika mali pake kwa usalama
unaotakiwa” alisema Masuka

No comments:
Post a Comment