Chadema wataka Katiba Jaji ya Warioba irejeshwe
MuroTV
SIASA
Chadema wataka Katiba Jaji ya Warioba irejeshwe

Chadema
imesema iwapo Tanzania inataka kunufaika na rasilimali zake na kushinda
vita vya kutetea utajiri wake inapaswa kwanza kurejesha katiba
iliyopendekezwa na Jaji Joseph Warioba na si vinginevyo.
Akitoa
msimamo wa chama kutokana na kile kinachoendelea baada ya kutolewa kwa
ripoti mbili za Rais kuhusu mchanga wa dhahabu, leo (Ijumaa) Katibu Mkuu
wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema suluhisho la kudumu katika
kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa ni kurejea katika katiba ya
wananchi.
“Chadema tunasema kuwa haya yote tunayoyapigia kelele itakuwa ni kazi bure iwapo haturejeshi hoja ya katiba mpya.
“Katiba
ya Warioba iliweka mapendekezo ya jinsi ya kulinda rasilimali za taifa
na kama tungefuata hayo yote hili la sasa halingepaswa kuwa na mjadala
mkubwa kiasi hiki,” amesema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.
Pia,
chama hicho kimeitaka CCM kujipima na kujitafakari kama kinafaa
kuendelea kuaminika kuongoza dola kutokana kushindwa kutetea vyema
rasimali za taifa kwa kuruhusu mikataba mibovu. Alisema Dk. Vicent Mashinji.
No comments:
Post a Comment