Madai ya mipango ya Rais Zuma kuhamia Dubai yaibuka Afrika Kusini
Nchini Afrika kusini kashfa mpya inatokota inayozingira madai ya rais Jacob Zuma ya kuzingatia kuhamia Dubai.
Barua
pepe hizo zimechapishwa na gazeti moja nchini Afrika kusini na
zinaonyesha uhusiano mkubwa kati ya rais wa Afrika kuisni Jacob Zuma na
familia yenye utata, Gupta, hususan kuhusu madai kwamba rais Zuma
anazingatia kuhamia Dubai.
Wakati chama tawala nchini Afrika
Kusini ANC kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani, barua pepe hizo
zinatarajiwa kuibua mjadala mkali kwani zinafichua mipango ya rais Zuma
ya kuhamia Dubai.
Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jela
Rais wa zamani Afrika Kusini ampinga Jacob Zuma
Thabo Mbeki aunga mkono wapinzani wa Zuma
Barua pepe hizo baina ya mwanawe Zuma, Duduzane, na vigogo wa
kampuni inayomilikiwa na familia tatanishi ya Gupta, zinashirikisha
barua moja iliyotumwa kwa familia ya kifalme nchini Dubai, ambapo Zuma
anasema angetaka kuwa na makao ya pili huko Dubai.
Madai hayo yanaibua mjadala wa iwapo rais Zuma anajiandaa kubwaga manyanga kwani chama cha ANC kinaonekana kumgeuka. Haki miliki ya pichaAFPImage caption
Zuma amekumbwa na kashfa nyingi ikiwemo ya makao ya Nkandla
Msemaji wa rais amepuuza barua pepe hizo kama uvumi na uchokozi.
Hayo
yakiarifiwa, ombi la kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma
limewasilishwa kwa kamati kuu ya chama cha ANC inayokongamana mjini
Pretoria.
Ni mara ya pili sasa ambapo waasi wa chama hicho wanawasilisha ombi hilo.
Wanachama wa ANC waandamana dhidi ya rais Zuma
Rais Zuma azuiwa kutoa hotuba Afrika Kusini
Muungano wa wafanyikazi wampiga marufuku rais Zuma
Hata hivyo, huenda wanchama wa kamati hiyo watiifu kwa rais Zuma wakaangusha mswada huo.
Kwa
sasa kesi inaendelea katika mahakama ya kikatiba ya iwapo wabunge wa
Afrika kusini watapiga kura ya siri ya kwa mswada wa kutokuwa na imani
na rais Jacob Zuma.
Kamati hiyo inatarajiwa kuamua atakayemridhi bwana zuma mwezi Desemba.
MADAI YA MIPANGO YA RAIS ZUMA KUHAMIA DUBAI YAIBUKA AFRICA KUSINI
Reviewed by Unknown
on
May 28, 2017
Rating: 5
No comments:
Post a Comment