KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA JINGINE KUELEKEA JAPAN
MuroTv
Korea Kaskazini yarusha kombora jingine kuelekea Japan
Korea Kaksazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu.
Kombora
hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya
kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan
kulalamika vikali.Wachanganuzi wanasema jaribio hilo ni ishara kwamba Korea Kaskazini inapiga hatua katika kuunda makombora yanayoweza kubeba mabomu.
- Marekani: Korea Kaskazini ilikusudia uchokozi
- Nyambizi ya Marekani yawasili Korea
Kikosi cha Jeshi la Marekani Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.
Waziri kiranja wa Japan Yoshihide Suga amewaambia wanahabari kwamba kombora hilo lilianguka katika eneo la bahari lililo kati ya visiwa vya Sado na Oki nchini Japan, katika eneo la pamoja la kiuchumi la visiwa hivyo viwili.

Jariibo hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo lilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.

Korea Kaskazini ina hazina kubwa ya makombora ya masafa mafupi aina ya Scud ambayo yaliundwa na Muungano wa Usovieti.
Makombora ya kisasa ya Scud yanaweza kufika umbali wa kilomita 1,000.
- Uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini
Korea Kaskazini ilisema jaribio la kwanza lilikuwa la kombora jipya lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.

Pyongyang imekuwa ikifanyia majaribio makombora kwa kasi sana, na wataalamu wanasema huenda inakaribia kufanikiwa kumiliki kombora la masafa marefu linaloweza kufikia maeneo ya Marekani bara.
- Marekani yaweka mtambo wa kulinda Korea Kusini
- 'Kifaa' cha Korea Kaskazini chashambuliwa na K. Kusini

- China yazindua meli kubwa ya kivita
- Ndege ya kwanza iliyoundwa China yapaa
No comments:
Post a Comment