KALA JEREMIAH BAADA YA MWAKYEMBE KUKATAZA WASANII KUIMBA SIASA
Burudani
Kala Jeremiah baada ya Mwakyembe kukataza wasanii kuimba Siasa
Hivi karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alisimama
Bungeni Dodoma akiwataka wasanii wajiepushe kuimba siasa badala yake
waelimisha jamii kauli ambayo imekuwa gumzo kwa wadau wa muziki.
Rapa staa Kala Jeremiah ambaye amekuwa na hisia tofauti na kauli ya Waziri Mwakyembe akisema ni ngumu kuitenganisha Siasa na Muziki.
“Siasa na Muziki ni ngumu
kuitenganisha kwa sababu hii kitu inaunganishwa na kitu kinaitwa Jamii.
Kuna vitu vitatu; siasa, muziki na jamii na jamii inakaa katikati ya
siasa na muziki.” – Kala Jeremiah.

No comments:
Post a Comment