SIMBA KUSHIRIKI MICHUANO YA CAF
Michezo
Simba imepata tiketi ya kushiriki michuano ya CAF leo

Simba waliingia katika mchezo huo wakiwa na jitihada za kuhakikisha wanapata ushindi na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kutoshiriki kwa muda mrefu kutokana na kutopata nafasi ya Ubingwa wa Ligi Kuu au wa FA.
Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na wabunge mbalimbali, Simba wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Simba yakifungwa na Fredrick Blagnon dakika ya 95 baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Abdi Banda na Shiza Kichuya dakika ya 120 aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Mbao kushika.

Goli pekee la Mbao FC ambao baada ya mchezo walimzonga muamuzi limefungwa na Ndaki Robert dakika ya 109, kiungo wa Simba James Kotei raia wa Ghana ndio alikuwa mchezaji bora wa mechi kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonesha, Simba sasa itashiriki michuano ya Kombe la shirikisho msimu wa 2017/2018.

No comments:
Post a Comment